Skip to main content

IOM imezindua wavuti Georgia kuwasaidia wanaotaka kuwa wahamiaji

IOM imezindua wavuti Georgia kuwasaidia wanaotaka kuwa wahamiaji

Wakati huohuo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linazindua wavuti nchini Georgia kuwasaidia wanaotaka kuwa wahamiaji kufanya uamuzi wa mipango yao ya kusafiri ng\'ambo kutafuta kazi.

Wavuti hiyo itakayoitwa www.informedmigration.ge ni moja ya miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya kwa ushirikiano na IOM, shirika la kazi duniani ILO na kituo cha kimataifa cha sera na maendeleo ya uhamiaji.

Lengo la mradi huo ni kutoa taarifa muhimu, za ufasaha, na zisizopendelea upande wowote za njia ambazo ni salama za uhamiaji na kuwapasha habari watu kuhusu athari za uhamiaji haramu na hatari ya kuwasafirisha watu kwa njia haramu.