Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la IOM linawasaidia waathirika tetemeko la ardhi Chile

Shirika la IOM linawasaidia waathirika tetemeko la ardhi Chile

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Chile linampango wa kuzisaidia familia 2100 zilizoathirika na tetemeko la ardhi la Februari 27.

Pia litahakikisha kwamba athari za tsunami katika majimbo ya kusini ya Maule na Biobio zinashughulikiwa. Tathimini ya awali ya serikali ya Chile inaonyesha kwamba nyumba laki mbili ziliharibiwa na hivyo watu wengi wanahitaji msaada wa dharura hususani wa malazi.

Mradi huo maalumu wa msaada wa IOM utachukua zaidi ya miezi mitatu na utajikita zaidi katika maeneo ya vijijini ambako msaada wa serikali unachukua muda mrefu kufika.