Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujenzi mpya wa Haiti hautofanikiwa endapo haki za binadamu zitapuuzwa

Ujenzi mpya wa Haiti hautofanikiwa endapo haki za binadamu zitapuuzwa

Mtaalamu binafsi wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Haiti leo amesema endapo haki za binadamu zitapuuzwa nchni humo basi ujenzi mpya hautofanikiwa.

amesema kama wahisani wa kimataifa ambao wataanza mkutano wao kesho hapa New York watajikita tuu katika kuangalia hali ya nje na ujenzi wa taasisi bila kuhakikisha haki za binadamu siku za usoni zinatekelezwa kwa raia wote, wanahatari ya kuweka mazingira ambayo yalifanya tetemeko la Januri kuwa na athari kubwa.

Misaada kwa Haiti bado inahitajika na OCHa inasema hadi sasa katika ombi la msaada wa dola bilioni 1.4 zilizopatikana ni asilimia 48 ambazo ni dola milioni 718.9. Forst amesema mkutano huo wa wahisani utakuwa muhimu sana kwa hatma ya Haiti na watu wake.