Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo vya usafiri kwa wetu wenye virusi vya HIV viondolewe:UNAIDS

Vikwazo vya usafiri kwa wetu wenye virusi vya HIV viondolewe:UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS na wabunge kutoka kote duniani wamezitaka serikali kuondoa vikwazo vya usafiri kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV.

Wito huo umetolewa leo katika mkutano wa 122 wa muungano wa wabunge unaofanyika mjini Bankok Thailand. Muungano huo wa wabunge na UNAIDS wanawataka wabunge wanaotoka nchi zinazoweka vikwazo kuchagiza kuondolewa kwa vikwazo hivyo.

Pia unawashawishi wabunge hao kuunga mkono kupitishiwa sheria za kuwalinda watu wenye HIV wasitengwe kutokana na hali yao. Kuna maeneo na nchi 52 ambazo zina aina fulani ya vikwazo hasa katika kuingia, kukaa na kuishi, vinavyozingatia hali ya mtu kuwa na virusi vya HIV.