Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabomu zaidi ya 1700 yameteguliwa na UNAMA nchini Afghanistan

Mabomu zaidi ya 1700 yameteguliwa na UNAMA nchini Afghanistan

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Afghanistan UNAMA umesema miezi miwili ya mwanzo ya mwaka huu wa 2010 umetegua mabomu zaidi ya 1,700.

Mabomu hayo ni yale yanayoweza kuzuru watu, na pia 135 ambayo yanaweza kulipua vifaru na zaidi ya silaha zingine laki moja na kumi zimeharibiwa . Na hivyo jamii 19 zimeachwa kuwa huru bila mabomu hayo na silaha zingine ambazo ni mabaki ya vita.

Wiki hii UNAMA itadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga mabomu ambayo ni tarehe 4 Aprili. Siku hii itatathimini mafanikio ya kimataifa katika kuangamiza mabomu na masalia ya silaha za vita.