Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tathimini yafanywa kuhusu WHO ilivyokabiliana na homa ya mafua ya H1N1

Tathimini yafanywa kuhusu WHO ilivyokabiliana na homa ya mafua ya H1N1

Kamati ya kujitegemea itathimini jinsi shirika la afya duniani WHO lilivyokabiliana na homa ya mafua ya H1N1.

Mshauri wa WHO wa homa ya mafua Daktari Keiji Fakuda ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Geneva kuwa tathimini ya mchakato huo itaangalia zaidi maandalizi na hatua zilizochukuliwa.

Pia itaangalia utekelezaji wa sheria za kimataifa za afya katika kukabiliana na ugonjwa huo. Na lengo kubwa ni kutathmini ni jinsi gani duania iliandaliwa na hatua ilizochukua kudhibiti mafua ya H1N1 na vipi dunia itahitaji ili kujiandaa vyema wakati magonjwa kama hayo yanapozuka. Dr Faduka anafafanua.