Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu limeelezea hofu yake juu ya sheria za uchaguzi Myanmar

Baraza la haki za binadamu limeelezea hofu yake juu ya sheria za uchaguzi Myanmar

Baraza la haki za binadamu leo limepitisha azimio la kuelezea wasiwasi wake juu ya sheria za uchaguzi nchini Myanmar.

Baraza hilo linasema sheria za uchaguzi zilizopitishwa na nchi hiyo zimeshindwa kujumuisha vipengee muhimu vitakavyohakikisha mchakato wa uchaguzi unajumuisha wanasiasa wa pande zote nchini humo.

Hofu yao kubwa ni kwamba sheria hizo hazifikii matarajio ya jumuiya ya kimataifa pia limetoa wito kwa serikali ya Myanmar kuhakikisha kwamba mchakato wa uchaguzi unakuwa huru, wazi na wa haki, ambao utaruhusu wapiga kura, vyama vyote na wadau wengine muhimu katika uchaguzi huo kushiriki.