Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usaili wa maombi ya ukimbizi barani Ulaya umebainika kuwa na dosari

Usaili wa maombi ya ukimbizi barani Ulaya umebainika kuwa na dosari

Utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR umebaini kuwa mfumo unaotumiwa na nchi za umoja wa Ulaya kusaili wanaoomba hifadhi ya ukimbizi una dosari.

Mtazamo unaochukuliwa na nchi wanachama wa jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa watu wanaoomba hifadhi ya ukimbizi wakati mwingine unakiuka sheria za kimataifa, ambapo waombaji sio wakati wote wanaweza kumudu usaili, na pia hawapewi muda wa kutosha kujiandaa na usaili au kuelezea madai yao.

UNHCR inasema mfumo huo unawaweka waombaji katika hatari, kwani ulinzi wanaohitaji hawapewi na wengine huenda wakarejeshwa waliokotoka na kuwa katika hatari ya kuuawa au kudhuriwa, kama anavyofafanua msemaji wa UNHCR