Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu karibu milioni moja wanakabiliwa na upungufu wa chakula nchini Uganda

Watu karibu milioni moja wanakabiliwa na upungufu wa chakula nchini Uganda

Mfumo wa tahadhari ya mapema ya baa la njaa FEWS Net umesema takribani watu laki tisa katika eneo la Karamoja Kaskazini Mashariki mwa Uganda wanakabiliwa na upunguvu wa chakula.

Mfumo huo unasema hali hii imechangiwa pakubwa na mvua za masika kutonyesha ipasavyo kwa miaka mine mfululizo nchini humo. Kwa mujibu wa FWAS Net asilimia 81 ya watu milioni 1.1 wanaokadiriwa kukumbwa na upungufu wa chakula nchini Uganda wako katika eneo la Karamoja.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limesema lina mpango wa kuanza tena kugawa chakula katika eneo hilo mwezi ujao wa April, kwani watu wamemeshatumia kile kidogo walichokuwa nacho.