Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ki-moon yuko ziarani Libya kuhudhuria mkutano wa jumuia ya nchi za kiarabu

Ban ki-moon yuko ziarani Libya kuhudhuria mkutano wa jumuia ya nchi za kiarabu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili nchini Libya leo asubuhi kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa jumuiya ya nchi za Kiarabu. Mkutano huo unaanza kesho.

Akizungumzia umuhimu wake bwana Ban amesisitiza juu ya hatua za hivi karibuni za mkutano wa mashariki ya kati uliokuwa na nia ya kufikia suluhu ya kudumu ya mgogoro wa eneo hilo.

Ameongeza kuwa majadiliano baiana ya Israel na Palestina ni lazima yazingatie maazimio ya mkutano,kwani ni njia muafaka na ya busara katika kutatua mzozo wa mashariki ya kati. Imefahamika kuwa ajenda kubwa ya mkutano wa jumuiya ya nchi za Kiarabu itakuwa ni mzozo wa mashariki ya kati.