Leo ni siku ya kumbukumbu ya waathirika wa biashara ya utumwa duniani

25 Machi 2010

Katika kuadhimisha siku ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema utumwa na matendo ya kitumwa bado yanaendelea katika sehemu mbalimbali duniani.

Katika ujumbe maalumu wa kukumbuka ukatili huo wa biashara ya utumwa bwana Ban amerejea wito wake wa jukumu la kimataifa kuahakikisha kwamba mifumo yote ya utumwa hatimaye inakomeshwa. Amesema ni lazima kuweka mazingira ambayo vitendo kama vya unyanyasaji na ukatili visiwe na nafasi.

Amesema kuadhimisha kumbukumbu hii ni njia moja ya kuwaenzi walioathirika na biashara hiyo kwa kutukumbusha haki ilivyokosekana hapo zamani, ili tuhakikishe ukiukaji kama huo wa haki za binadamu asilani hautorudiwa tena.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud