Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetoa wito wa Afghanistan kufuta sheria inalowalinda wahalifu wa kivita

UM umetoa wito wa Afghanistan kufuta sheria inalowalinda wahalifu wa kivita

Umoja wa Mataifa leo umetoa wito kwa Afghanistan kuifuta sheria yenye utata ya msamaha ambayo inatumika kama ngao ya kutowahukumu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wa kivita.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo sheria ya maridhiano na msamaha ilipitishwa na bunge la Afghanistan mwaka 2007 na ikachapishwa kimyakimya kwenye gazeti rasmi la nchi hiyo Desemba 2008.

Sheria hiyo imekosolewa vikali na makundi ya kupigania haki za binadamu ya Afghanistan na ya kimataifa baada ya kutangazwa na vyombo vya habari mapema mwaka huu. Mwakilishi wa Afghanistan kwenye tume ya haki za binadamu Nora Niland amesema ni tatizo kwa Afghanistan na kwa nchi kuweza kuachana na migogoro ni lazima iweze kukabiliana na matatizo yaliyopita.