Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inachunguza madai ya kuzuka ugonjwa wa ndui nchini Uganda

WHO inachunguza madai ya kuzuka ugonjwa wa ndui nchini Uganda

Shirika la afya duniani WHO limekuwa likifanya kazi kwa karibu na wizara ya afya ya Uganda kufuatilia visa vinavyodaiwa kuwa ni ugonjwa wa ndui.

Baada ya uchunguzi na kufuatilia kwa karibu sasa imebainika kuwa ungonjwa unaodaiwa kuwa ni ndui kumbe ni tetekuanga, na ulizuka nchini Uganda wiki tatu zilizopita. WHO inasema tukio hilo sio kubwa la kutisha lakini imewapa taarifa hii mpya wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Ugonjwa wa tetekuwanga umekuwepo katika nchini mbalimbali na mara nyingi huwaathiri watoto wadogo. WHO ikishirikiana na nchi mbalimbali imekuwa katika mikakati ya chanjo ya ugonjwa huo ambao kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa.