Uharibifu wa misitu duniani umepungua lakini bado ni tatizo kwa nchi nyingi

25 Machi 2010

Hali ya uharibifu wa misiti duniani imepungua kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita,lakini ukataji miti unaendelea katika nchi nyingi.

Katika ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, inasema matokeo ya kupungua kwa misitu mingi ni kutokana na hifadhi ya misitu kutumiwa kwa kilimo.

FAO inakadiria kwamba duniani kote karibu ekari milioni 13 za misitu zimekuwa aikitumika kwa mambo mengine au kupotea kila mwaka katika kipindi cha mwaka 2000 na 2010.Tofauti na miaka ya 1990 ambapo ekari milioni 16 zilikuwa zikipotea kila mwaka. Amerika ya Kusini na Afrika ndio kwa muongo uliopita ndio walioongoza kwa kupotea kwa misitu kila mwaka.

Asia kwa upande mwingine imearifiwa kuwa na ongezeko kubwa la misitu kwa miaka kumi iliyopita, hasa ni kwa sababu ya program maalumu ya upandaji miti China, India na Viet Nam.

Zaidi ya wataalamu 900 kutoka nchi 178 wameshiriki katika tathmini ya kimataifa ya rasilimali ya misitu kwa mwaka huu wa 2010. Ripoti kamili ya tathimini hii itatolewa mwezi Octoba mwaka huu

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter