Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma ya maisha ya sokwe barani Afrika bado iko njia panda

Hatma ya maisha ya sokwe barani Afrika bado iko njia panda

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP na jeshi kubwa la kimataifa la polisi INTERPOL wamesema hatma ya sokwe barani Afrika bado iko njia panda.

Wamesema endapo hakutachukuliwa hatua za kulinda makazi ya sokwe hao na kuzuia ujangili basi sokwe wengi katika msitu wa Congo watatoweka kwa kiasi kikubwa katikati ya mwaka 2020. Makadirio ya awali yaliyofanywa na UNEP mwaka 2002 yalisema asilimia kumi ya sokwe hao ndio itakayobaki ifikapo 2030.

Lakini makadirio hayo ni makubwa ukilinganisha na kasi ya kutoweka kwa sokwe hao hasa kwa kuwa shughuli kama uwindaji haramu, uchimbaji madini, uzalishaji wa makaa ya mawe, homa ya ebola na mahitaji ya nyama ya porini yameongezeka. Maelfu ya sokwe wameshauawa kutokana na sababu hizo.