Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya malazi imewafikia waathirika milioni moja wa tetemeko Haiti

Misaada ya malazi imewafikia waathirika milioni moja wa tetemeko Haiti

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC linasema robo tatu ya watu milioni 1.3 wasio na makazi kutokana na tetemeko nchini Haiti sasa wamepata msaada wa vifaa vya malazi kama mahema na nguzo za ujenzi.

Hadi sasa watu waliopokea msaada huo unaosambazwa na mashirika yapatayo 50 ni laki 976,775. Msaada huo unaosimamiwa na IFRC una leongo la kuwafikia watu asilimia 100 ifikapo Mei mosi unapoanza msimu wa mvua nchini Haiti.

Mratibu wa IFRC Gregg McDonald amesema kila wiki wanawapa msaada watu laki moja tangu kutokea kwa tetemeko hilo zaidi ya miezi miwili iliyopita.