Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi Sudan unajongea na hofu imeanza juu vya vitisho kwa wapinzani

Uchaguzi Sudan unajongea na hofu imeanza juu vya vitisho kwa wapinzani

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake juu ya taarifa kwamba baadhi ya wajumbe wa upinzani na wafuasi wao wanatishwa nchini Sudan.

Taarifa hiyo inasema wengine wanadhalilishwa, kukamatwa na hata kuwekwa kizuizini zikiwa zimesalia wiki chache tuu kabla ya uchaguzi wa Rais na wabunge uliopangwa kufanyika mwezi ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari hapa New York msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema hofu nyingine waliyonayo ni kuhusu idadi ndogo ya wakimbizi wa ndani walioandikishwa kupiga kura kwenye jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.

Lingine ni changamoto za kiufundi kama njia ya kusafirisha vifaa vya uchaguzi katika maeneo ambayo hayafikiki na jinsi ya kuwapata na kuwapa mafunzo maelfu ya wafanyakazi watakaotumika kwenye uchaguzi.

Zaidi ya watu milioni 16 ambao ni takribani asilimia 80 ya watu wanaokadiriwa kuwa na umri wa kupiga kura wamejiandikisha na mchakato wa uteuzi wa wagombea umekamiliaka.