Skip to main content

Hali ya haki za binadamu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado ni mbaya

Hali ya haki za binadamu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado ni mbaya

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wakimbizi wa ndani amesema hali ya haki za binadamu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado haijaimarika.

Akiwasilisha ripoti yake mjini Geneva amesema hali bado ni mbaya ikiwa ni pamoja na katika maeneo ambayo hayajaathirika na mapigano. Unyanyasaji na ukiuaji mkubwa wa haki unaofanywa na majeshi ya ulinzi na usalama unatia hofu.

Mwakilishi huyo Walter Kaelin amesema ukatili dhidi ya wanawake na hususani kubakwa, na kubakwa na magenge ya watu kunkofanywa na wanajeshi na raia kunaendelea