Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa

Leo ni siku ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa

Leo ni siku ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa duniani, kauli mbiu ikiwa ni miaka 60 ya huduma kwa ajili ya maisha na usalama wako"

Katibu mkuu wa shirika la hali ya hewa duniani Michel Jarraud amesema miongo ijayo utabiri, tathmini na huduma ya hali ya hewa itakuwa muhimu sana katika kuhakikisha kuna chakula cha kutosha, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuchangia katika maendeleo.

Na kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo mwaka 2009 umetajwa kuwa ndio mwaka wa tano uliokuwa na joto sana katika historia tangu kuanza kuwekwa kwa kumbukumbu za hali ya hewa mwaka 1850.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba mwaka 2000 hadi 2009 kulikuwa na joto sana kuliko 1990-1999.