Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kimataifa wa kuongeza nafasi za kazi utasaidia uchumi:ILO

Mpango wa kimataifa wa kuongeza nafasi za kazi utasaidia uchumi:ILO

Afisa wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi Helen Clark amesema mpango wa kazi wa kimataifa wa shirika la kazi duniani ILO utasaidia kufungua njia kwa nchi nyingi zilizoathirika na mdororo wa uchumi kuanza kujerea katika hali ya kawaida.

Bi Clark ambaye alikuwa akihutubia bodi ya wakurugenzi wa ILO wanaokutana mjini Geneva, amesema sio kitu rahisi kutaka kuweza kuwa na mamilioni ya nafasi za kazi kila mwaka ili kuhakikisha kiwango cha ukuaji wa uchumi hakishuki.

Lakini amesema ili kuhakikisha malengo ya milenia yanafikiwa ya kupunguza njaa na umasikini uliokithiri kwa nusu ifikapo 2015 katika nchi nyingi, basi ni lazima nafasi za kazi ziwepo, hususani kwa nchi zinazotaka kutoka kwenye hali mbaya ya mdororo wa kiuchumi.