Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na Ujerumani kusaidia waathirika wa kubakwa nchini Sierra Leone

IOM na Ujerumani kusaidia waathirika wa kubakwa nchini Sierra Leone

Mpango wa serikali ya Ujerumani unaofadhili shirika la kimataifa la uhamiaji IOM unatoa msaada wa kiufundi na kitaalamu kwa mradi maalumu nchini Sierra Leone.

Mradi huo ni wa kushughulikia athari mbaya za ukiukaji wa haki za binadamu na uvunjaji wa sheria za kimataifa uliotekelezwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone mwaka 1991 hadi 2002.

Mradi huo unalengo la kuwasaidia wanawake 650 ambao walibakwa na kunyanyaswa kimapenzi kwa kuwapa mafunzo na pia fedha taslim dola 500 ili kuanzisha miradi ya kuwasaidia na kujiendeleza kielimu. Jean Philippe ni afisa wa IOM