Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afghanistan inaongoza kwa wanaoomba ukimbizi nchi za Magharibi

Afghanistan inaongoza kwa wanaoomba ukimbizi nchi za Magharibi

Imebainika kwamba idadi ya Waafghanistan wanaoomba hifadhi ya ukimbizi katika nchi za magharibi zilizoendelea kiviwanda imeongezeka karibu mara mbili mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hilo ndio kundi kubwa kabisa la watu wanaohitaji hifadhi.Mwaka jana pekee Waafghanistan elfu 26,800 waliomba ukimbizi nchi za magharibi ikiwa ni asilimia 45 zaidi ya mwaka 2008 .

Na hii inawafanya kushika namba moja duniani ya watu wanaoomba ukimbizi wakifuatiwa na Wairaq na Wasomali. Nchi zote hizo tatu zinakabiliwa na vita visivyokwisha ambavyo kila uchao vinakatili maisha ya watu. Nchi nyingine zilizo na wakimbizi wengi nje ni Urusi, Uchina, Nigeria na Serbia