Skip to main content

Sierra Leone yachukua hatua kali kupambana na ufisadi

Sierra Leone yachukua hatua kali kupambana na ufisadi

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mahusiano ya kujenga amani nchini Sierra Leone UNIPSIL inasema nchi hiyo imechukua hatua kali katika miezi michache iliyopita kupambana na ufisadi.

Michael Von der Schulenburg akitoa taarifa leo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu shughuli za ofisi yake, amese mambo matatu muhimu yanayokuwa kikwazo kwa amani ya Sierra Leone ni ukosefu wa ajira kwa vijana, biashara haramu ya dawa za kulevya na ufisadi.

Amesema katika kupambana na rushwa hatua mbalimbali zimechukuliwa, watu kadhaa wamekamatwa na kuhukumiwa kwa makosa ya ufisadi, sio tuu kwa maafisa wa chini bali hata viongozi wa ngazi za juu wa serikali.

Ameongeza kuwa mwezi Januari mwaka huu mkurugenzi wa mamlaka ya mapato alisitishwa kazi kufuatia uchunguzi wa tume ya kuzuia rushwa .Na tarehe 11 Machi waziri wa zamani wa afya alihukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa makosa ya ufisasi. Naye katibu wa kudumu na waziri wa uvuvi wa nchi hiyo, 15 ya mwezi huu wa Machi alishitakiwa kwa makosa ya ufisadi na kuachishwa kazi.

Amesema Umoja wa Mtaifa uko tayari kutoa msaada wa kiufundi kuisaidia Sierra Leone ili isikose kutendewa haki na wawekezaji kwa ajili ya maendeleo ya taifa.