Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wameshawishi kiongozi wa waasi kujiunga katika mchakato wa amani

Umoja wa Mataifa wameshawishi kiongozi wa waasi kujiunga katika mchakato wa amani

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ameshawishi kiongozi wa waasi wa Sudan kujiunga na mchakato wa amani.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan amezungumza na kiongozi wa kundi muhimu la waasi lililomeguka Darfur lenye makao yake nchini Ufaransa katika juhudu zake za kuchagiza mchakato wa amani kwenye jimbo hilo la Sudan.

Mwakilishi huyo bwana Ibrahimu Gambari anayeongoza mpango wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID alikuwepo mjini Paris Ufaransa kukutana na Abdul Wahid Al-Nour kiongozi wa kundi la Sudanese Liberation Army (SLA)

Kundi la SLA awali lilikuwa ndani ya muungano wa makundi ya waasi yaliyokuwa yakipigana na majeshi ya serikali ya Sudan kwenye jimbo la Darfur. Bwana Gambari amemshawishi Al-Nour na muungano wa vikosi vyake kujiunga na mchakato wa amani.

Pia ameomba kuwepo na ushirikiano baina ya vikosi vya Al-Nour na vikosi vya UNAMID, na amemuomba Al-Nour asaidie kurahisisha shughuli za mashirika ya ugawaji wa misaada ya kibinadamu kuwafikiwa watu wanaohitaji misaada.

Gambari akiwa Paris pia amekutana na maafisa wa serikali ya Ufaransa i, mabalozi na pia mshauri wa masuala ya Umoja wa Mataifa na Afrika kwa Rais Nicolas Sarkozy.