Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya haki za binadamu yatathmini ripoti ya Katibu Mkuu wa UM

Tume ya haki za binadamu yatathmini ripoti ya Katibu Mkuu wa UM

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inatathmini ripoti ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon inayohusu eneo la Syria la Golan linalokaliwa na Israel.

Ripoti hiyo inaitaka Israel kuzingatia maazimio ya Umoja wa mataifa na kutangaza kuwa haustahili na ni haramu uamuazi wa kuweka sheria na utawala wake katika eneo la Golan linalokaliwa nchini Syria, na maazimio hayo yanaitaka Israel kupindua uamuzi huo.

Ripoti hiyo pia ina maoni mbalimbali ya nchi wanachama kuhusu mtazamo wa kukaliwa maeneo mbalimbali ya Mashariki ya kati. Maoni hayo ni kutoka Morocco, Pakistan, Algeria, Egypt na Syria yenyewe. Navi Pillay ni mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa