Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa tano kuhusu ukuaji wa miji na makazi umeanza Brazil

Mkutano wa tano kuhusu ukuaji wa miji na makazi umeanza Brazil

Mkutano wa tano kuhusu hali ya miji na makazi umefunguliwa leo mjini Rio de Janeiro nchini Brazili.

Mkutano huo uliofunguliwa na Rais Lula Da Silva wa Brazil umeandaliwa kwa ushirikiano wa serikali ya Brazil a shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-Habitat. Mkutano huo hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa lengo la kutafuta suluhu ya ongezeko la matatizo ya ukuaji wa miji.

Kauli mbiu mwaka huu ni "Haki ya kuishi mjini na kuondoa mgawanyiko".

Mkurugenzi mkuu wa UN-Habitati Dr Anna Tibaijuka anafafanua umuhimu wa mkutano huo na lengo lake.