Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedha zinahitajika katika kufufua uchumi na maendeleo ya Darfur

Fedha zinahitajika katika kufufua uchumi na maendeleo ya Darfur

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan amesema hali ya walioathirika na machafuko ya Darfur ni mbaya na juhudi kubwa zinahitajika kuleta maendeleo ya jimbo hilo.

Mwakilishi huyo bwana Ibrahim Gambari amesema wakimbizi wengi wa ndani wanapatiwa huduma kama chakula, elimu na masuala ya afya lakini fedha zinahitajika ili kuinua uchumi na hali ya maisha ili wakimbizi hao waweze tena kujitegemea. Ameyasema hayo kwenye mkutano wa wahisani mjini Cairo Misri.

Inakadiriwa kuwa watu laki tatu wameuawa kwenye machafuko ya Darfur na wengine milioni 2.7 wamekuwa wakimbizi. Ahadi ya mamilioni ya dola imetolewa kwenye mkutano huo katika kulisaidia jimbo la Darfur.