Magonjwa ya kuambukiza yamedhibitiwa Port-au-Prince Haiti

Magonjwa ya kuambukiza yamedhibitiwa Port-au-Prince Haiti

Shirika la afya duniani WHO linasema hakujakuwa na ongezeko lolote la magonjwa ya mlipuko katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince.

Kuzinduliwa kwa kampeni ya chanjo ambayo hadi sasa imeshawafikia watu laki nne kumesaidia sana kupunguza mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza. Kitengo cha afya cha shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wiki hii kimezindua mpango wa kuwasaidia wagonjwa.

Mpango huo unawarejesha nyumbani wale walio tayari kutoka hospitali, kuwahamisha wanaotakiwa kupelekwa kwenye hospitali zingine na wale wanaotakiwa kwenda kwenye vituo vya ushauri nasaha.

Hata hivyo kitengo hicho kimesema kinahitaji msaada na ushirikiano kutoka kwa jamii hasa kuwasaidia waathirika ambao wanataka kurejea katika maisha ya kawaida.