Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kwanza wa kidini kujadili ukimwi utaanza Jumatatu

Mkutano wa kwanza wa kidini kujadili ukimwi utaanza Jumatatu

Viongozi wa kidini na kiroho kutoka sehemu mbalimbali duniani watakunata nchini Uholanzi kuanzia jumatatu ijayo tarehe 22 Machi hadi 23 kwa mkutano wa kwanza kabisa kuwahi kufanyika wa viongozi wa kidini kujadili ukimwi.

Mkutano huo utawaleta pamoja viongozi 40 wakimwemo Bahai, Mabuda, Wakristo, wahindu, Wayahudi, Waislam , Singasinga pamoja na wakurugenzi wakuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na ukimwi UNAIDS na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA.

Wengine ni mabalozi wa ukimwi wa Uholanzi na Sweden, viongozi na wawakilishi wa mitandao ya watu wanaoishi na virusi vya HIV na mashirika mengine yaliyo msitari wa mbele katika vita dhidi ya ukimwi.