Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa unawasaidia waathirika wa maporomoko Madagascar

Umoja wa Mataifa unawasaidia waathirika wa maporomoko Madagascar

Umoja wa Mataifa na washirika wake wanapeleka misaada ya dharura kwa watu walioathirika na maporomoko ya ardhi yaliyotokana na hali mbaya ya hewa na mvua kubwa nchini Madagascar.

Maporomoko hayo ymelikumba eneo la mwambao wa mashariki mwa Madagascar na yalianza tangu tarehe 10 ya mwezi huu. Takwimu rasmi zinasema hadi sasa watu 54 wamefariki dunia kutokana na maporomoko hayo.

Wengine elfu 98 wameathirika na  laki nne wakiachwa bila makazi. Nyumba zaidi ya elfu tatu zimesombwa na maporomoko hayo, na serikali imelazimiaka kufunga shule sita na vituo vya afya viwili. Elizabeth Brys ni msemaji wa OCHA anafafanua kuhusu misaada