Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji safi na salama ni haki ya kila mtoto wasema Umoja wa Mataifa

Maji safi na salama ni haki ya kila mtoto wasema Umoja wa Mataifa

Taarifa ya pamoja iliyotolewa kwa ajili ya kuazimisha siku ya maji duniani itakayokuwa Jumatatu ijayo tarehe 22 Machi inasema maji safi ni haki ya kila mtoto.

Taarifa hiyo iliyotolewa na wanaharakati wa Umoja wa Mataifa wa kupigania haki za binadamu, wataalamu wa maji, usafi, afya, elimu na ukatili dhidi ya watoto inasema, ukosefu wa maji safi na salama unatishia uhuru wa haki za binadamu.

Wanaharakati hao wametoa wito wa kutoa kipaumbele kwa watoto na kuongeza juhudi za kuhakikisha kwamba ndoto ya kupata maji safi, salama na usafi inatimia.