Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kombe la dunia litasaidia mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi

Kombe la dunia litasaidia mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema michuano ya kombe la dunia la mpira wa miguu itakayofanyika mwezi June mwaka huu nchini Afrika ya Kusini itatoa fursa ya kuliangalia upya suala la ubaguzi wa rangi.

Amesema mashindano hayo ni mwanya mzuri wa kuangalia suala la ubaguzi katika michezo na kuifanya michezo kutofumbia macho suala hilo, pia mauaji ya kibaguzi na mifumo minge isiyovumilika katika jamii.

Wanaharakati wa kupigania haki za binadamu wanasema ubaguzi wa rangi sio tatizo la jana, bali ni changamoto ya leo, kwani watu wanaendelea kupoteza maisha kutokana na misingi ya ubaguzi wa rangi katika mabara yote duniani.

Navi Pillay ameyasema hayo katika taarifa maalumu ya kuazimisha siku ya kutokomeza ubaguzi wa rangi ambayo itasherehekewa siku ya jumapili tarehe 21machi.