Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo baiana ya Israel na Palestina ni chachu ya amani Mashariki ya kati

Mazungumzo baiana ya Israel na Palestina ni chachu ya amani Mashariki ya kati

Mkutano wa kujadili hatma ya amani ya mashariki ya kati uliokuwa unafanyika Moscow Urusi umemalizika.

Mkutano huo ulijumuisha Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton, mwakilishi wa muungano wa Ulaya Catherine Ashton na mwakilishi maalumu wa mashariki ya kati Tony Blair.

Kimsingi mkutano huo umesema suala la kuchagiza mazungumzo ya amani ni muhimu sana ili kuziwesha Israel na Palestina kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

Mkutano huo unaamini kuwa masuala muhimu kama makazi ya walowezi, na kuundwa kwa taifa la Palestina yatawezekana ikiwa pande hizo mbili zitazingatia watakayoafikiana katika miezi 24 ya majadiliano. Akiondoka Moscow kuelekea Israel na Palestina Katibu mkuu Ban Ki-moon amesema mkutano wao ulikuwa wa mafanikio.