Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi lingine la waasi Sudan latia saini mkataba wa amani Doha

Kundi lingine la waasi Sudan latia saini mkataba wa amani Doha

Maafisa wa serikali ya Sudan leo wametia saini mkataba wa kusitisha vita kwa miezi mitatu na kundi lingine la waasi la Liberation and Justice Movement (LJM).

Kundi hilo ni muungano wa makundi mengine madogomadogo ya waasi. Na mkataba huo umesainiwa mjini Doha Qatar. Makubaliano hayo yanatarajiwa kufumgu milango kwa ajili ya majadiliano ya kisiasa katika kuelekea amani ya kudumu.

Kundi hilo la LJM limetia saini wiki chache tuu baada ya kundi lingine la waasi na lenye ushawishi mkubwa kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan la Justice and Equality Movement (JEM) kusaini mkataba wa amani na serikali ya Rais Bashir.