Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulio la roketi dhidi ya Israel

Umoja wa Mataifa walaani shambulio la roketi dhidi ya Israel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la roketi lililovurumishwa leo dhidi ya Israel kutoka ukanda wa Gaza.

Shambulio hilo limemuua raia mmoja wa Israel na bwana Ban amesisitiza kuwa vitendo vya ghasia vya aina hiyo havikubaliki. Roketi hilo limearifiwa kuanguka katika eneo la Netiv Ha'assera Kibbutz kusini mwa Israel na aliyeuawa ni mfanyakazi wa kigeni wa shamba.

Ban amesema vitendo vya kigaidi kama hivyo vinaenda kinyume na sheria za kimataifa.

Shambulio hilo limefanyika katika mkesha wa mkutano wa mashariki ya kati ambao Ban Ki-moon anatazamiwa kushiriki mjini Moscow ukijumuisha pia Urusi, Marekani na muungano wa Ulaya.