Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon kukutana kuzungumza na viongozi wa Urusi Moscow

Ban Ki-moon kukutana kuzungumza na viongozi wa Urusi Moscow

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili mjini Moscow kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Urusi kuhusu mahusiano katika muundo wa Umoja wa Mataifa.

Pia atashiriki kwenye mkutano wa mawaziri  wapatanishi wa mashariki ya kati unaojumuisha pia urusi, Marekani, Umoja wa Mataifa na muungano wa Ulaya. Kesho bwana Ban anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Sergei Nesterenko viongozi hao watajadili suluhisho la matatizo ya kimataifa na nafasi ya Umoja wa Mataifa kuchukua jukumu la kuwa mratibu mkuu. Miongoni mwa matatizo hayo ni hali ya mashariki ya kati, amani ya kudumu Iraq, Sudan , suala la uzalishaji wa nyuklia, upokonyaji wa silaha na misaada ya kibinadamu kupitia mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.