Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya misaada yanajitahidi kufikia malengo Haiti

Mashirika ya misaada yanajitahidi kufikia malengo Haiti

Mashirika ya misaada yanafanya kila juhudi kugawa misaada inayohitajika kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Haiti ili kufikia malengo ya tarehe mosi May.

Shirikisho la Chama cha kimataifa cha msalaba mwekundu na jumuiya ya mwezi mwekundu (IFRC) limearifu kwamba mpaka sasa wameshagawa msaada wa malazi kwa familia zaidi ya elfu 60 kabla ya kufikia tarehe ya malengo mwezi May.

Msemaji wa IFRC Pablo Medina anasema idadi hiyo ni asilimia 80 ya familia laki moja na themanini walizopanga kuzisaidia. Pablo Medina anasema shirika lake pia linatoa msaada wa aina nyingine kwa waaathirika wa tetemeko kama chanjo dhidi ya magonjwa , msaada wa maji na ujenzi wa vyoo.

Ameongeza kuwa bado kuna changamoto kubwa mbele yao ambayo ni pamoja suala la ardhi, kuondoa kifusi na eneo la makazi ya kudumu.