Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kina mama Sierra Leone yaiuzia WFP chakula

Jumuiya ya kina mama Sierra Leone yaiuzia WFP chakula

Jumuiya ya kina mama wakulima wa mbogamboga nchini Sierra Leone iitwayo Koinadugu women\'s vegetable farmers cooperative, kwa mara ya kwanza imeliuzia mchele shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Mchele huo tani 25 umenunuliwa kupitia mradi maalumu ujulikanao kama nunua kwa ajili ya maendeleo, na mchele huo utatumiwa na WFP katika mradi wake wa kugawa chakula katika shule mbalimbali .

Mchele huo unatosheleza kuwalisha watoto 3800 wa shule za msingi kwa miezi mitatu. Na mchele huo ni awamu ya kwanza ya jumla ya tani 500 za chakula ambazo WFP ina mpango wa kununua mwaka huu kutoka mashirika 10 tofauti nchini Sierra Leone.