Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahaka ya ICTR imepupilia mbali rufaa ya Leonidas Nshogoza

Mahaka ya ICTR imepupilia mbali rufaa ya Leonidas Nshogoza

Kitengo cha rufaa cha mahakama ya kimataifa inayohukumu kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ICTR iliyoko Arusha Tanzania leo imetupilia mbali rufaa ya wakili wa zamani aliyetaka hukumu yake ibadilishwe au kifungo kipunguzwe.

Leonidas Nsogoza alihukumiwa kwenda jela miezi kumi mwezi Julai mwaka jana baada ya kukutwa na hatia ya kukutana na kutoa taarifa zilizolindwa za mashahidi jambo ambalo ni kinyume na amri ya mahakama.

Katika rufaa yake bwana Nsogoza aliomba mahakama imfutie mashitaka na kumwacha huru au ipitie upya hukumu yake na kumpunguzia kifungo, lakini kitengo cha rufaa leo kimesalia na hukumu ileile aliyopewa na kusema haiwezi kutengua uamuzi huo kwani Nsogoza alishindwa kuthibitisha kuwa alionewa.

Hata hivyo imepongeza kwa muda aliotumikia jela na kusema aachiliwe wakizingatia kuwa alijisalimisha mwenyewe katika mahakama hiyo Februari mwaka 2008 na amekuwa jela kwa wakati wote huo.