Wanasayansi wanakutana kujadili biashara ya vitu vitokanavyo na mimea
Wanasayansi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanakutana Doha Qatar kujadili biashara ya kimataifa ya viumbe vilivyoko katika hatari ya kutoweka Flora na Fauna.
Wanasayansi hao wanatathmini namna ya kudhibiti biashara ya viumbe hivyo vya porini na mazao yatokanayo na mimea hiyo mfano mbao ambazo hutengeneza vitu kama vyombo vya muziki , dawa za saratani, urembo kama rangi za kupaka mdomoni,na dawa za kung'arisha viatu.
Vingine ni pamoja na ubani, vipodozi, mafuta uzuri (perfumes) na vitu vingine vingi vitokanavyo na mimea ya porini. Kwa kufanya hivyo wanasayansi hao wanaamini wataweza kulinda mimea hiyo iliyoko katika hatari kubwa ya kutoweka.