Haiti bado inahitaji msaada kurejea katika maisha ya kawaida

15 Machi 2010

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Haiti bado inakabiliwa na hali ngumu na matatizo makubwa , na juhudi kubwa za msaada zinahitajika kuikwamua katika hali hiyo.

Amsesema ingawa kumepigwa hatua katika usambazaji wa misaada ya dharura kama chakula na maji, bado nchi hiyo inahitaji fedha kwa ajili ua kujenga upya shule, miundombinu, masuala ya barabara, michezo na nishati.

Ameongeza kuwa serikali ya Haiti itahitaji msaada wa kimataifa ili iweze kulipa mishahara ya walimu, polisi, madaktari na manesi, pia wafanyakazi wengine wa serikali. Ameongeza kuwa  cha msingi ni kuendelea kuwa na mshikamano na kuchagiza wahisani katika mkutano wa Machi 31 utakaofanyika New York.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter