Ban Ki-moon aitaka Myanmar kujumuisha wapinzani katika mfumo wa kisiasa

11 Machi 2010

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejea wito wake kwa serikali ya Myanmar kuhakikisha pande zote zinajumuishwa katika mchakato wa kisiasa katika kuelekea uchaguzi.

Amesema kufanya hivyo kutaufanya uchaguzi uwe huru na wa haki na watu wote wa Myanmar akiwemo kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi anaweza kuwa huru kushiriki. Kauli hiyo imefuatia tangazo la serikali ya Myanmar kutangaza sheria mpya za uchaguzi wakijiandaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa ya bwana Ban dalili zinaonyesha hadi sasa mchakato wa kisiasa nchini humo haujafikia matarajio ya jumuiya ya kimataifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter