Skip to main content

Mafuriko yawafanya maelfu kukosa makazi zambia na Msumbiji

Mafuriko yawafanya maelfu kukosa makazi zambia na Msumbiji

Mvua kumbwa zinazoendelea kunyesha kaskazini mwa Msumbiji na kaskazini mwa zambia zimesababisha vina vya maji katika mito kujaa na hivyo serikali kuamua kufungua maji ya bwawa la Kariba nchini Zimbabwe na Kahora Bassa nchini Msumbiji.

Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA linasema pia mvua hizo zimesababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya maeneo. Juzi serikali ya Msumbiji ilitangaza hali ya tahadhari baada ya baadhi ya maeneo kukumbwa na mafuriko.

Watu elfu 13 wamehamishiwa kwenye maeneo ya usalama, na nchini Zambia inakadiriwa kuwa familia 800 zimeathirika na mafuriko hayo na zingine 150 zimelazimika kupelekwa kwenye kambi za muda zilizoandaliwa na serikali.