Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timor Mashariki sasa yajivunia amani na utulivu baada ya machafuko

Timor Mashariki sasa yajivunia amani na utulivu baada ya machafuko

Rais wa Timor ya Mashariki Jose Ramos Horta leo ameuambia Umoja wa mataifa katika baraza la haki za ninadamu mjini Geneva kuwa, nchi yake sasa inajivunia amani na utulivu baada ya machafuko.

Amesema licha ya matatizo ya kiuchumi waliyonayo kwa sasa, wanajitahidi kukabiliana nayo polepole na wanafurahia miaka mitatu isiyo na bugudha na uchumi unaanza kutengamaa taratibu.

Nchi hiyo ilikumbwa na machafuko makubwa mwaka 2006.