Skip to main content

Matokeo ya awali nchini Iraq yamuweka pazuri waziri mkuu

Matokeo ya awali nchini Iraq yamuweka pazuri waziri mkuu

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge yaliyotolewa na tume ya uchaguzi nchini Iraq, yanaashiria kwamba waziri mkuu Nour al-Maliki anashinda katika majimbo mawili ya Washia kusini mwa Iraq.

Matokeo hayo ni ya kwanza kutolewa baada ya uchaguzi wa kihistoria kufanyika nchini humo Jumapili iliyopita. Matokeo hayo yaliyotangazwa leo ynaonyesha muungano wa chama kinachoongozwa na bwana Maliki katika jimbo la Babil kinaongoza kwa kura karibu 14,000 na kwenye jimbo la Najaf kinaongoza kwa kura 7,000.

Matokeo hayo ni theluthi tuu ya ya kura zote katika majimbo hayo. Katika majimbo mengine kura bado zinahesabiwa ili kupata matokeo.