Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zimbabwe inahitaji msaada wa haraka wa chakula

Zimbabwe inahitaji msaada wa haraka wa chakula

Wito wa msaada wa fedha umerejewa tena ili kuwasaidia haraka maelfu ya Wazimbabwe wnaohitaji msaada wa chakula.

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC limesema kutokana na takwimu za karibuni kabisa watu wanaokadiriwa kuwa milioni 2.17 nchini Zimbabwe kwa sasa wanahitaji msaada wa chakula.

Hata hivyo imeelezewa idadi hiyo itaongezeka kutokana na mavuno hafifu yanayotarajiwa mwaka huu. Katika baadhi ya maeneo nchini humo hali ya upungufu wa chakula ni mbaya mno amesema Bi Emma Kundishora katibu mkuu wa chama cha msalaba mwekundu nchini Zimbabwe .

Ameongeza kuwa katika aeneo la Masvingo kwa mfano mvua hazikunyesha kwa wakati, na mimea imekufa.

Mathew Cochrane ni afisa wa OCHA nchini Zimbabwe.