Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa shughuli zake Somalia

WFP kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa shughuli zake Somalia

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa chakula duniani WFP leo umesema uko tayari kutoa ushirikiano kwa uchunguzi binafsi dhidi ya shughuli zake za misaada ya chakula nchini Somalia.

Wakati huohuo shirika hilo limesema halitoshirikiana tena na wakandarasi watatu waliotajwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia masuala ya Somalia. Wakandarasi hao wakidaiwa kujihusisha na biashara ya silaha.

Mkurugenzi mkuu wa WFP Josette Sheeran amesema hadhi ya shirika lao ni muhimu sana na watatathimini na kuchunguza kila suala lililotajwa na ripoti hiyo. Amesema wako tayari kutoa ushirikiano kwa uchunguzi wowote utakaofanyika kuhusu kazi yao Somalia, kwani kila siku WFP wanafanya kazi katika mazingira magumu kuhakikisha Wasomali wenye njaa wanapata chakula.