Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi 90 wa FDLR wauawa mashariki mwa Congo DRC

Waasi 90 wa FDLR wauawa mashariki mwa Congo DRC

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUC umesema majeshi ya serikali mashariki mwa Congo yamewaua wanamgambo 90 wa kihutu kutoka Rwanda katika mashambulizi yaliyoanza mwezi uliopita.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinaliunga mkono jeshi la serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika operesheni ijulikanayo kama "Amani Leo" ambayo inawalenga wapiganaji wa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) katika majimbo ya Kivu yanayopakana na Rwanda.

Kivu ya Kaskazini operesheni mbili zimekamilika katika maeneo ya Kashebere na Mayengara na matokeo yake wanajeshi 23 wa FDLR wameuawa , 40 wamejisalimisha na vituo vyao viwili vimesambaratishwa.