Ban Ki-moon alaani hatua ya Israel kuongeza makazi ya Walowezi

10 Machi 2010

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mipango ya Israel ya kuongeza kujenga makazi ya walowezi 1,600 katika eneo linalokaliwa la Wapalestina wanaodai kuwa na taifa lao.

Kauli hiyo inaungana na matamshi ya makamu wa Rais wa Marekani Joe Baiden aliyoitoa mapema wiki hii. Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirk, Ban ki-moon leo amesema analaani mipango hiyo ya nyumba zitakazojengwa mashariki mwa Jerusalem na wizara ya mambo ya ndani ya Israel.

Ameongeza kuwa makazi hayo ya walowezi ni kinyume na jukumu la Israel katika mkataba wa amani, na inahatarisha juhudi zozote za mipango ya amani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter