Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chakula cha msaada kwa mamilioni ya Wasomali chatoweka

Chakula cha msaada kwa mamilioni ya Wasomali chatoweka

Karibu nusu ya chakula cha msaada kilicholengwa kuwafikia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa nchini Somalia kimetowekea mikoni mwa wahandisi mafisadi, wanamgambo wa Kiislam na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Taarifa hii ni kutokana na ripoti ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambayo bado haijatolewa. Ripoti hiyo inalaumu matatizo ya uzambazaji mbaya wa chakula katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika ambayo imeghubikwa na vita na adha kwa watu wake kwa karibu miongo miwili.

Vitendo vya utekaji na mauaji vimetawala na usalama mdogo unawafanya maafisa wa Umoja wa Mataifa kushindwa kusafiri katika baadhi ya maeneo kuangalia shughuli za ugawaji wa chakula. Watu takribani milioni 3.7 ambao ni karibu nusu ya watu wote nchini Somalia wanahitaji msaada.